Header Ads

UJUE MCHAICHAI NA FAIDA ZAKE


Ni wengi wanaoutumia na  kuufahamu mchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwamajani haya yana faida kubwa  kiafya Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda  vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa  mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya
ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.

Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:


KINGA DHIDI YA SARATANI
Tafiti mbalimbali zimeonyesha
kuwa kwenye kila gram 100 ya
mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya
ugonjwa wa saratani. Mwaka
2006, timu ya watafiti kutoka
Chuo kikuu cha Gurion, Israel
waligundua mchaichai una
uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.
MMENG'ENYO WA CHAKULA
-Husaidia umeng’enyaji wa
chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha
utaratibu wa mmeng’enyo wa
chakula na pia hutibu
magonjwa ya kuhara na
maumivu ya tumbo ikiwamo
kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa
kuondoa uchafu mwilini
Katika matibabu,
unatibu magonjwa
mengi ikiwemo
kushusha joto, hasa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na
malaria kali.
KUSAFISHA FIGO NA MKOJO
Mchaichai pia una kazi ya
kusafisha figo ambayo kazi yake
kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta
mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali
kiwandani na hivyo mwili
kushindwa kuziondoa na
baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo
saratani.
Figo inapokuwa safi na imara,
hata kazi nyingine kama
kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi kwani mkojo unapozidi
kuwa mchafu mtu hujikuta
akivimba mwili na wakati
mwingine kufikia hata hatua ya
kupoteza maisha.
MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia kina
mama ambao wanaumwa na
tumbo kipindi cha hedhi, ambao
wengi wao huchukulia kama
chango.
“Unapokunywa mchaichai,
unawezesha kusafisha mirija ya
uzazi na hivyo kuwezesha damu
kupita kwa urahisi,”
MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU
vilevile mchaichai una
kazi ya kusafisha damu, hasa
kwa watu ambao wamekuwa na
tabia ya kupata magonjwa ya
ngozi kama mapele na kutoka
majipu
KUZUIA KUHARISHA
Mchaichai pia unaelezwa kuwa
ni dawa ya kuzuia kuharisha
ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya
protozoa anayesababisha
ugonjwa huo.
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia
majani ya mmea huu kwa muda
mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji
kwani husaidia katika kulegeza
nyonga ambazo hubana katika
kipindi cha ujauzito na kufanya
njia kuwa ndogo kuwezesha
mtoto kupita,
WENYE VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa hasa na
vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia
kuondoa gesi ambazo huwapata
mara kwa mara.
HUONGEZA CD4
Kwa wagonjwa wa ukimwi,
mchaichai unaelezwa kuwa
huongeza CD4 na inashauriwa
kuwa ni vyema mgonjwa wa
aina hiyo akapendelea kutumia
zaidi mchaichai kuliko majani
ya chai.

No comments:

Powered by Blogger.